Niite
Jinsi Biblia inavyosema katika zama hizi za UKIMWI
J. Larko Steiner(Author)
Strategies for Hope Trust (Publisher)
Published on 1. April 2011
Book
Paperback/Softback
76 pages
978-1-905746-18-7 (ISBN)
Description
Kitabu hiki kina masomo 20 ya Biblia kuhusu mada kama vile kujamiiana na nidhamu yake, ndoa, tumaini, uongozi wa kanisa, msamaha, watu wanaoishi na WU, hofu na wasiwasi, unyanyapaa, watoto, na kifo, huzuni na maombolezo. Kila somo linatakiwa kuchukua muda kati ya dakika 90 na masaa mawili kukamiiika. Kitini cha TUMEITWA KUHUDUMIA kinajumuisha matendo, vijitabu vyenye kuhusisha matendo na miongozo midogo kuhusu mambo yanayohusu VVU na UKIMWI, vilivyoandaliwa kwa matumizi ya viongozi wa kanisa, hasa kwa nchi zilizo Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Madhumuni ya mambo yaliyomo ni kuwawezesha wachungaji, mapadre, watawa wa kike na wa kiume, walei viongozi wa kanisa na waumini wao pamoja na jamii ili waweze: - Kutafakari na kuelewa kiroho, kitheolojia, kimaadili, kiafya, kijamii na kimatendo madhara ya janga la VVU na wito wa Kikristo wa kuitikia kwa huruma. - Kushinda unyanyapaa, ukimya, ubaguzi, kukataa, woga na kukataa kubadilika, hali ambazo zinazuia kanisa na jamii katika kukabiliana na mambo yanayohusu VVU na UKIMWI kwa ukamilifu zaidi.
- Kuwaongoza waumini wao na jamii katika mchakato wa kujifunza na kubadilika kutakakopelekea kwenye matendo na mienendo ya kikanisa ili kuwasaidia watu binafsi, familia na jamii ili kupunguza kuenea kwa VVU na kupunguza athari za janga la VVU. TUMEITWA KUHUDUMIA ni wazo la Wadhamini wa Mikakati ya Kuleta Matumaini, ambao wanatayarisha na kutoa vitabu na video vinavyohamasisha mbinu madhubuti na michakato ya kijamii ya kuhudumia, kusaidia na kuzuia VVU na UKIMWI katika nchi zinazoendelea duniani, hasa zilizoko Afrika chini ya Jangwa la Sahara. TUMEITWA KUHUDUMIA inatekelezwa kupitia mchakato wa kimataifa, shirikisho la muungano wa makanisa, na taasisi nyingine za kidini, miundo ya kimataifa ya makanisa, wachapishaji, wasambazaji na washika dau wengine.

More details
Series
Language
Other
Place of publication
Oxford
United Kingdom
Illustrations
22 line drawings
Dimensions
Height: 297 mm
Width: 210 mm
Thickness: 5 mm
Weight
222 gr
ISBN-13
978-1-905746-18-7 (9781905746187)
Copyright in bibliographic data and cover images is held by Nielsen Book Services Limited or by the publishers or by their respective licensors: all rights reserved.
Schweitzer Classification
Persons
Askofu William Mchombi ni Askofu wa Dayosisi ya Anglikana Zambia Mashariki. Ana digrii kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda na Chuo Kikuu cha Western Cape, Afrika ya Kusini. Kasisi Dennis Milanzi ni kasisi wa parish na Meneja Mradi katika Dayosisi ya Anglikana Zambia Mashariki, ambako pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Watoto Kanisa la Anglicana Mt. Paulo. Kasisi Canon Alfred Sebahene ni Mkuu wa Kitivo cha Chuo cha Theolojia na Mafunzo ya Dini katika Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania. Ana Digrii ya Pili kutoka Chuo Kikuu cha Middlesex, Uingereza. Joyce Larko Steiner ni Meneja Mradi wa Haki za Binadamu, Jinsia na Programu za WU katika Baraza la Kikristo la Ghana. Ana digrii ya BA (Rons) katika Ustawi wa Jamii na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika fani ya masuala ya VVU na UKIMWI. (Mhariri)
Author
Editor
Illustrated by
Translation
Content
Neno la utangulizi na Askofu William Mchombo. Utangulizi. Uaminifu wa Mungu. Kanisa na janga la UKIMWI. Familia. Mitazamo na matendo binafsi. Mambo yanayomsumbua mwanadamu. Sifa ya mwanadamu. Kiambatanisho: Mambo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI.